Pages

Ads 468x60px

Friday, August 29, 2014

RASMI ALONSO ATUA BAYERN MUNICH,ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI.



                                Kiungo mpya wa wa Bayern munich Xabi Alonso.

Hatimae mabingwa wa ligi kuu ya Ujerumani klabu ya Bayern Munich wamekamilisha usajili wa kiungo Jabi Alonso kutoka Real Madrid uhamisho uliowagharimu kiasi cha Euro milioni 10.
Mabingwa hao wa Bundesliga wamethibitisha kupitia tovuti yao kwamba kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 amesaini mkataba  wa kuichezea timu hiyo inayofundishwa na kocha Pep Guardiola hadi mwaka 2016.
Alonzo ambaye jumatano ya wiki hii alitangaza kustaafu soka la kimataifa aliwasilisha barua ya kutaka kuondoka Santiago Bernabeu baada ya kusajiliwa  wa kiungo Toni Kroos kutoka Bayern Munich na Jemes Rodriguez kutoka Monaco ya Ufaransa.
                              Kiungo mpya wa Bayern Munich Xabi Alonso.

Alonzo amesajiliwa ili kuiongezea nguvu safu ya kiungo wakati ya Bayern Munich baada ya kuumia kwa wachezaji Javi Martinez, Bastian Schweinsteiger na Thiago Alcantara.

                                      Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment