Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 28, 2014

HATIMAE JEZI NAMBA 7 KUVALIWA NA DI MARIA MACHESTER UNITED.

 Angel di Maria akiwa na kocha Louis Van Gaal wakati akitambulishwa ndani ya uwanja wa Old Traford.

Klabu ya manchester United chini ya kocha mkuu Louis Van Gaal imemkabidhi mshambuliaji wake mpya Angel Di Maria jezi namba 7 ambayo kwa muda mrefu imekosa mvaaji baada ya Antonio Valencia kuomba abadilishiwe jezi hiyo na kurejea jezzi yake ya zamani ya namba 25.

Di Maria mabye amesajiliwa wiki hii akitokea Real Madrid ya Hispania anataraji kucheza mchezo wake wa kwanza mwishon i mwa wiki ambapo Manchester United itakuwa ikicheza na Barnley kwenye pambano la ligi kuu ya England.

Licha ya kuanza vibaya katika msimu huu wa Ligi kiungo wa Manchester United raia wa Hispania Juan Mata amesema anamatumaini ujio wa Di Maria klabuni hapo utasaidia kuongeza nguvu kikosi chao ambacho msimu hakishiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya.

Kwa upande wake Di Maria amesema amejisikia fuaraha kupewa jezi hiyo imewahi kuvaliwa na baadhi ya wachezaji waliowahi kufanya makub wa klabuni hapo huku akidokeza kuwa Cristiano Ronaldo alimwambia faida kubwa atakayoipata akiichezea Manchester Unite.
miongoni mwa wachezaji waliowahi kuvaa jezi no,7  ndani ya Manchester United ni George Best  Bryan Robson, Eric Cantona, David Beckham ,Cristiano Ronaldo,Michael Owen na Antonio Valencia ambaye hatahivyo aliomba abadilishiwe.



                             Di Maria akionyesha jezi no,7 atakayokuwa akiivaa akiwa Manchester United.

                            Kifaa  kipya cha manchester United Angel Di Maria akiwa katika pause.

No comments:

Post a Comment