Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 20, 2014

MARTINO ATANGAZA KIKOSI CHA KWANZA AKIWA KOCHA WA ARGENTINA.

        Gerardo Martino katikati hapa akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Kocha mpya wa timu ya taifa ya Argentina Gerardo Martino ametangaza kikosi chake cha kwanza tangu achukue mikoba ya Alejandro Sabella aliyeachia ngazi baada ya kuifikisha nchi hiyo kwenye hatua ya fainali za mwaka huu za kombe la dunia na kufungwa na Ujerumani goli 1 kwa 0.

Kikosi hicho kipya cha Martino kitapambana na Ujerumani kwenye mchezo wa kirafiki mwezi ujao mjini Duesseldorf.

Katika kikosi hicho cha Argentina chenye wachezaji 23 Martino amewaacha wachezaji watatu wanaocheza ligi ya ndani ambao ni kiungo Fernando Gago,mlindamlango Agustin Orion anayekipiga na klabu ya Boca Juniors na winga wa Newell's  Maxi Rodriguez.

Kocha Gerado Martino anataraji kukikamilisha kikosi hicho Sept 3 baada ya kuchezwa kwa mchezo baina ya Boca na Newells.
 Messi siku ya fainali ya kombe la dunia baada ya Argentina kufungwa na Ujerumani goli 1 kwa 0 mwaka huu nchini Brazil
Kikosi kilichotangazwa na kocha Tata Martino kinawachezaji wafuatao:-
Goalkeepers: Sergio Romero (Sampdoria), Mariano Andujar (Napoli)
Defenders: Pablo Zabaleta (Manchester City), Federico Fernandez (Napoli), Ezequiel Garay (Zenit St Petersburg), Marcos Rojo (Manchester United), Hugo Campagnaro (Inter Milan), Martin Demichelis (Manchester City), Jose Basanta (Fiorentina)
Midfielders: Javier Mascherano (Barcelona), Lucas Biglia (Lazio), Ricardo Alvarez (Inter Milan), Augusto Fernandez (Celta Vigo), Angel Di Maria (Real Madrid), Enzo Perez (Benfica)
Forwards: Lionel Messi (Barcelona), Gonzalo Higuain (Napoli), Sergio Aguero (Manchester City), Rodrigo Palacio (Inter Milan), Ezequiel Lavezzi (Paris St Germain)

                                 Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment