Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 14, 2014

PIGO BAYERN MUNICH,JAVI MARTINEZ AUMIA VIBAYA KUKAAA NJE YA DIMBA MIEZI 4.




Javi Martinez akitolewa uwanjani kwa machela baada ya kuumia kwenye mchezo wa jana dhidi ya Borussia Dortmund.

Kiungo wa  mabingwa wa ligi kuu ya Ujerumani Bayern Munich Javi Martinez  leo anataraji kufanyiwa upasuaji wa goti baada ya kumia kwenye pambano la jana baina ya timu yake na Borrusia Dortmund kuwania kombe la DFL Super Cup ambapo kikosi chake kilifungwa magoli 2 kwa 0.

Mchezaji huyo raia wa Hispania amesema madaktari wa timu yake wamemwambia kuwa goti lake limeadhirika kwa asilimia 99 kutokana na  kukumbana na mlinzi wa Borussia Dortmund Marcel Schmelzer muda mfupi baada Borussia kupata goli la kuongoza.

                           Javi Martinez akipata msaada kutoka kwa madaktari wa Fc Bayern Munich.

Javi Martinez  ambaye ni mchezaji wa zamani wa Atletico Bilbao imethibitika kuwa  atakaa nje kwa muda miezi minne kupatiwa matibabu ya jeraha la goli alilolipata kwenye mchezo huo wa jana.

Katika mchezo huo magoli ya Borussia Dortmund chini ya kocha Jurgen Klopp yalifungwa na wachezaji Henrikh Mkhitaryan dakika ya 23 pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang dakika 62 na kuiwezesha  timu yao kushinda  taji hilo.

                           Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment