Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 7, 2014

VALENCIA YANASA SAINI YA MLINZI WA KIJERUMAN MUSTAFI KUTOKA SAMPDORIA.





                               Shkodran Mustafi akiwa na mmoja wa viongozi wa Valencia.

 Mlinzi wa klabu ya Sampdoria  na timu ya taifa ya Ujerumani Shkodran Mustafi amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Valencia kwa mkataba wa miaka mitano  na leo alhamisi anatarji kufanyiwa vipimo vya afya.

Mustafi ambaye akikuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kiklixchotwaa ubingwa wa kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil kwakuifunga Argentina  goli 1 kwa 0 mara baada ya kufanyiwa vipimo hivyo leo atatambulishwa rasmi kwa vyombo vya habari.

Taarifa kutoka kwenye tovuti ya klabu ya Valencia inayoshiriki ligi kuu ya Hispania imethibitisha kufikia makubaliano na Sampdoria  na mkataba wake utamalizika june 30 mwaka 2019.
Mustafi mwenye umri wa miaka 22 anatarajiwa kukamilisha vipimo vya afya  leo saa 9.45 am kisha  kutambulishwa  kwa vyombo vya habari saa 10.00

                        Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment