Pages

Ads 468x60px

Friday, August 15, 2014

TONY PULIS ABWAGA MANYANGA KUINOA CRYSTAL PALACE.





                                          Tony Pulis.

Wakati ligi kuu ya England ikitaraji kuanza kesho aliyekuwa kocha wa timu ya Crystal palace Tony Pulis  kwakile kilichotajwa kutoridhishwa na mipango ya usajili ya klabu hiyo msimu huu.
Pulis mwenye umri wa miaka 56 jana jioni alifanya mazungumzo na mwenyekiti wa timu hiyo Steve Parish nakufikia uamuzi huo kutokana na kutowezeshwa  kusajili kati ya wachezaji aliokuwa anawataka kama Gylfi Sigurdsson na  Steven Caulker.
Katika msimu huu wa usajili timu hiyo imesajili wachezaji wane pekee wawili ambao ni Fraizer Campbell na  Martin Kelly ndio walionunuliwa kwa huku wawili Chris Kettings na  Brede Hangeland wakijiunga na kikosi kwa uhamisho huru.
Crystal Palace ambayo kesho itaanza ligi kuu ya England kwakucheza na Arsenal itakuwa chini ya kocha msaidizi  Keith Millen hadi pale kocha mkuu atakapopatikana.
Pulis ambaye aliteuliwa kuwa kocha wa bora wa  ligi kuu ya England  mwezi wa tano mwaka jana wakati anaifundisha Stock City alikuchukua nafasi Ian Holloway mwezi wa 11 nakuisaidia placed kumaliza katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi.

                            Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment