Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 27, 2014

CRYSTAL PALACE YAMTANGAZA WARNOCK KUWA KOCHA MPYA.



                     Neil Warnock kocha mpya wa Crystal Palace.

Klabu ya soka ya Crystal Palace imemtangaza Neil Warnock kuwa kocha wao mpya  kwa mkataba wa miaka miwili  kuchukua nafasi ya Tony Pulis aliyeachia ngazi juma lililopita.
Warnock mwenye umri wa miaka 65 aliwahi kuifundisha Palace kati ya mwaka 2007 na 2010  na sasa atakuwa akisaidiana na kocha msaidizi Keith Millen ambaye  alipewa jukumu la kocha mkuu wa muda baada ya Tony Pulis kuachia ngazi.
Kocha huyo mpya ameahidiwa  na uongozi wa Palace kuwa atapewa fungu la kufanya usajili kabla ya dirisha kufungwa jumatatu ijayo.
Ikiwa chini ya kocha msaidizi Keith Millen  tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi kuu ya England  Crystal Palace  ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Arsenal kwakufungwa magoli 2 kwa 1 ikiwa ugenini kabla ya kufungwa magoli 3 kwa 1 na West ham huku ikishinda goli 3 kwa 0 dhidi ya Walsall kwenye mzunguko wa pili wa Capital one Cup.
                              Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment