Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 13, 2014

ROONEY NAHODHA MPYA WA MANCHESTER UNITED.




                                                                         Wayne Rooney.
Kocha wa Manchester United Lous Van Gaal amemteua mshabuliaji Wayne Rooney kuwa nahodha mpya wa  mabingwa hao mara 20 wa ligi kuu ya England ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa 2014/2015.
Rooney mwenye umri wa miaka 28 amechukua kitambaa hicho cha unahodha kilichoachwa na mserbia Nemanja Vidic aliyejiunga na Inter Milan katika msimu huu wa usajili barani Ulaya.
Rooney ambaye ameteuliwa jana  baada ya Manchester United kushinda magoli 2 kwa 1 dhidi ya Valencia kwenye mchezo ya kirafiki atakuwa akisiadiwa jukumu la unahodha na Darren Fletcher
Akizungumza mara baada ya kupewa jukumu hilo la unahodha Rooney amesema hiyo ni heshima kubwa kwake nakuahidi kuwaongoza vyema wachezaji wenzake sambamba na kuendelea kucheza  soka kwa kiwango cha juu zaidi.


Wayne Rooney hapa ni mwaka 2009.

August 2004: Akiwa na umri wa miaka 18- Rooney alijiunga na Man united akitokea Everton kwa ada ya paundi milioni 27.
September 2004: Alifunga hat-trick yake ya  kwanza  kwenye mchezo dhidi ya Fenerbahce  ambapo Man U ilishinda magoli 6 kwa 2 ukiwa ni mchezo wake wa kwanza kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya.
November 2006:  alisaini mkataba wa miaka 2 kurefusha nakumfanya asalie Old Traford  hadi  mwaka 2012.
August 2009: Rooney alifunga goli la 100 akiwa na United kwenye pambano la ligi kuu ya England dhidi ya Wigan Athletic.
April 2010: Akateuliwa  na chama cha soka cha England kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka sambamba na ile tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka kutoka kwa waandishi wa habari.
October 2010:  Alizua mgogoro na United baada ya kutangaza kuwa anataka kuihama timu hiyo kabla ya kubadili kauli hiyo  na siku chache baade akasaini mkataba mpya.
May 2013: Aliyekuwa kocha mkuu wakati huo Sir Alex Ferguson akampiga benchi Rooney kwenye mchezo wa mwisho kuhitimisha msim u katika dimba la Old Traford kwakusema nyota huyo ameomba kuondoka  kwa mabingwa hao mara 20 wa BPL.
September 2013: Rooney akawa mchezaji wan ne kufunga  kufikisha magoli 200 akiwa na United  katika ushindi wa magoli 4 kwa 2 katika michuano ya Chapions league ambapo mashetani hao wekundu walikuwa wakicheza na B ayer Leverkusen  na hapo Rooney akawa ameungana na wakongwe wa Mani United kama Sir Bobby Charlton, Denis Law  na  Jack Rowley.
February 2014:  Akasaini mkkataba wa miaka minne uliomfanya apokee msharaha wa paundi laki tatu kwa wiki  na mkataba huo utamalizika mwishoni mwa msimu wa 2018/2019.

                          Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment