Shirikisho la soka nchini TFF leo limetoa ratiba ya michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajia kuanza tarehe 20 ya mwezi wa tisa ikishirikisha timu 14 .
Ratiba
hiyo imezingatia michuano ya Chalenji itakayochezwa mwezi Novemba, usajili wa
dirisha dogo ambao utaanza Novemba 15 hadi Desemba 15, ushiriki wa klabu za
Azam na Yanga kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa afrika na Kombe la
Shirikisho.
Mechi
za ligi msimu ujao zitachezwa wikiendi tu ili kuongeza msisimko na kuwapa fursa
washabiki wengi zaidi kuhudhuria, katikati ya wiki imeachwa wazi kwa ajili ya
mechi za Kombe la FA (Federation Cup), Vilevile kutakuwa na mechi Boxing Day na
siku ya Mwaka Mpya.
Ratiba
hiyo inaonesha mabingwa watetezi azam fc wataanza na wageni wa ligi Polisi
Morogoro wakati Yanga wao wataanza ugenini dhidi ya Mtibwa Suger.
Simba sc
wao wataanza dhidi ya Coastal Union jijini Dare s salaam wakati Ndanda Fc wao
watafungua dhici ya Stand United mkoani Shinyanga.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment