Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 6, 2014

WEBB ASTAAF SASA KUWA MKURUGENZI WA WAAMUZI.





                                   Howard Webb.



Webb kwenye mchezo wa fainali ya kombe la dunia 2010 nchini Afrika ya kusini kati Uholanzi na Hispania.

Mwamuzi maarufu barani Ulaya raia wa Uingereza Howard Webb amestaafu kazi hiyo na kuwa mkurugenzi mkuu wa michezo ya kimataifa .

Webb mwenye umri wa miaka 43 alianza kazi ya uamuzi wa soka tangu mwaka 1989  nakutambulishwa rasmi katika ligi kuu ya England mwaka 1998  kabla ya kusimamia michezo mbalimbali ya klabu bingwa Ulaya na kombe la dunia.

Webb ambaye ni askari mstaafu wa Uingereza mchezo wake wa kwanza akiwa mwamuzi wa ligi kuu ya England  ulikuwa mwezi wa 10 mwaka 2003 kabla ya kujumuishwa kwenye orodha ya waamuzi wa shirikisho la soka dunia Fifa miaka miwili baadae.

Mwamuzi huyo mkongwe  majukumu yake yatakuwa ni pamoja na kuwa mkufunzi wa waamuzi na masuala mbalimbali ikiwa na kufundisha mambo mbalimbali kwenye jamii yanayohusu uamuzi wa soka.

Akizungumza mara kustaafu Webb amesema anajisikia furaha kuanza ukurasa mpya wa maisha yake baada ya taaluma yake ya  uamuzi wa soka  kwa miaka 25 nakuongeza kuwa amejifunza mengi kwenye fani hiyo.

                                Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment