Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 10, 2014

ARSENAL YAIADHIBU MAN CITY 3 -0. COMMUNITY SHIELD.


   Kikosi cha Arsenal kikifurahia ngao ya jamii leo baada ya kuifunga Manchester City.

Timu ya soka ya Arsenal leo imeibuka mbabe kwenye mchezo wa Community Shield uliochezwa kwenye uwanja wa Wembley baada ya kuifunga Manchester City magoli 3 kwa 0.
Arsenal walianza kujipatia goli la kwanza kupitia kwa Santi Carzola dakika ya 21 kabla ya Arony Ramsey kufunga goli la pili dakika ya 42  kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na mchezaji Yaya Sanogo.
Hadi nusu ya kwanza inamalizika Arsenal ilikuwa Mbele kwa magoli hayo mawili huku Manchester City ambao ni mabingwa wa ligi kuu ya England msimu uliopita wakiwa hawana kitu.

Kipindi cah pili kilianza kwa kila upande kufanya mashambulizi lakini Arsenal ndio waliokuwa  na bahati hii leo baada ya kujipatia goli la 3 na la mwisho kunako dakika ya 61 lililotiwa  kimiani na mfaransa Oliver Giroud.

Hadi dakika 90 zinamlizika Arsenal 3 Manchester City 0.

Mchezo huo wa ngao ya jamiii ni kiashinshio cha kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya England 2014/2015 unaotaraji kuanza wiki ijayo Augost 16 mwaka huu wa 2014.


          Kikosi cha Arsenal kikiwa katika picha ya pamoja baada ya kutwaa ngao ya jamii leo.

   Santi Carzola,Alexis Sanches katikati nahodha wa leo Arteta  wakiwa wameshikilia ngao ya jamii .

              Kushinda raha sana hapa vijana wa Arsenal wakifurahia ngao ya jamii.

                                     Hekaheka zilivyokuwa leo pale Wembley.

      Teknolojia ambayo ilitumika katika kombe la dunia nchini Brazil sasa kutumika katika ligi kuu ya England msimu huu unaoanza mwishoni mwa juma hili. 



Sat
16/08/14












Sun
17/08/14


Mon
18/08/14




                                                       Mkule.blogsport.com





No comments:

Post a Comment