Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 7, 2014

XAVI ATANGAZWA KUWA NAHODHA MPYA WA FC BARCELONA.




Xavi Hernandez wapili kutoka kushoto akiwa na wenzake,Iniesta wakwanza kushoto,Sergio     Busketwakwanza kulia akifuatiwa na Messi.

Timu ya Fc Barcelona imemtakanza kiungo Xavi Hernandez kuwa nahodha mpya kuchukua nafasi ya Carles Puyol aliyestaafu hivi karibuni.

Xavi mwenye umri wa miaka 34 ameanza kazi nhiyo rasmi na atafaa kitambaa hicho katika msumu mpya wa ligi 2014/2015 na atakuwa akisaidiwa na Andres Iniesta ambaye pia atapokezana na Leonel Messi na Sergio Buskets.

Msimu uliopita Victor Valdes alikuwa nahodha namba tatu  baada ya Puyol na Xavi lakini mlindamlango huyo ameondoka klabuni hapo baada ya kumalizika kwa mkataba wake na Wakatalunia hao.

Xavi ambaye anakaribia kufikisha michezo 500  ya La liga akiwa na Fc Barcelona tangu mwaka 1998 ameshatwaa mataji 7 ya ligi kuu ya Hispania  na mataji matatu ya klabu bingwa Ulaya na mawili ya Copa del Reys.
                                      Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment