Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 20, 2014

SWANSEA CITY YAKAMILISHA USAJILI WA FERNANDEZ KUTOKA NAPOLI.


                                           Federico Fernandez.

Klabu ya Swansea City imethibitisha kukamilisha usajili wa mlinzi wa timu ya Napoli ya Italia Federico Fernandez kwa mkataba wa miaka minne.
Fernandez mwenye umri wa miaka 25 amejiunga kwa uhamisho huru na kufaulu vipimo vya Afya alivyofanyiwa jumatatu ya wiki hii kisha kupewa jezi namba 33.
Raia huyo wa Argentina  akiwa kwenye kikosi cha Swansea City atashinania namba na nahodha wa kikosi hicho Ashley Williams, Jordi Amat na  Kyle Bartley kwenye nafasi ya Ulinzi.
Mlinzi huyo anatarajia kuingia mmoja kwa mmoja kwenye kikosi cha Swansea City kitakachoivaa Barnley juammosi ya wiki hii katika mfulululizo wa ligi kuu ya England iliyoanza mwishoni mwa juma lililopita.
Kusajiliwa kwa Fernandez ni utekelezaji wa kocha wa Swansea city Garry Monk baada ya wiki iliyopita kukaririwa akisema anamhitaji mlinzi huyo  kwakuwa atamfaa huku akitaja umri wake wa miaka 25 unafaa kwa Swansea City.
Akiwa na Napoli Fernandez ameisaidia timu hiyo kutwaa taji la Copa Italia msimu uliopita huku ikimaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A.
Pia mlinzi huyo alishiriki kwenye fainali za mwaka huu za kombe la dunia ambapo Argentina iliambulia nafasi ya pili baada ya kufungwa na Ujerumani goli 1 kwa 0 kwenye mchezo wa fainali.

Katika timu ya taifa Fernandez amecheza michezo minne  pekee.

                                   Mkule.blogsport.com.


No comments:

Post a Comment