Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 20, 2014

RODRIGUEZ AFUNGUKA BAADA YA KUFUNGUA AKAUNTI YA MAGOLI REAL MADRID.




Nyota mpya wa timu ya Real Madrid raia wa Colombia Jemes Rodriguez  amesema anamatumaini makubwa ya kufunga magoli kadri atakavyopata nafasi katika msimu wake wa kwanza akiwa na klabu hiyo ya Hispania.
Jemes ambaye alifunga goli lake la kwanza akiwa na Real usiku wa  kuamkia leo kwenye mchezo wa Spanish Super cup dhidi ya Atletico Madrid uliomalizika kwa sare ya goli 1 kwa 1 ameeleza kuwa na furaha baada ya kufungua ukurasa wake wa kwanza wa magoli akiwa timu hiyo.
Nyota huyo ambaye amesajiliwa kutoka Monaco ya Ufaransa baada ya kuonyesha kiwango kikubwa kwenye fainali za kombe la dunia  mwaka huu  nchini Brazil amebainisha kuwa anaimani kuwa Cristiano Ronaldo atarejea kiwango chake baada ya kuzongwa na majeruhi.
Katika mchezo huyo wa kuashiria kuanza kwa ligi kuu ya Hispania itakayoanza  jumamosi ya wiki hii Rodriguez alichukua nafasi ya Ronaldo  ambaye  alipumzishwa na kocha Carlo Ancelotti amesema mreno huyo anataraji kufaniwa uchunguzi.
 Rodriguez akijaribu kumiliki mpya kwenye mbano la usiku wa kuamkia leo dhidi ya Atletico madrid.

Nyota wa Atletico Madrid wakiongozwa na Raul Garcia' mbele wakishangilia goli usiku wa kuamkia leo kwenye pambano dhidi ya Real Madrid.

 Nyota wa Real madrid Gareth Bale akijaribu kuwatoka wachezaji wa Atletico Madrid  kwenye pambano la Spanish Super cup lililomalizika kwa sare ya goli 1 kwa 1.

                            Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment