Pages

Ads 468x60px

Friday, August 15, 2014

KIKOSI CHA MBEYA CITY CHAANZA ZIARA YA MICHEZO YA KIRAFIKI MKOANI RUKWA.





                                                                Kikosi cha Mbeya City.
Kikosi cha timu ya Mbeya City cha mkoani Mbeya leo kimeanza riaza ya siku tano mkoani Rukwa ambapo kikiwa huko kitacheza michezo mbalimbali ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi unaotaraji kuanza mwezi ujao.

Katibu mkuu wa timu hiyo Emmanueli Kimbe amesema kikosi chote kimesafiri na kikiwa huko  wanataraji kuzindua matawi mbalimbali ya timu yao ambayo ilifanya vyema katika msimu uliopita na kufanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara nyuma ya mabingwa Azam Fc na Yanga.

Kimbe amesema ziara hiyo pia ina lengo la  kulipa fadhika kwa mashabiki wao waliokuwa msitari wa mbele kuishambilia timu hiyo katika michezo mbalimbali ya ligi kuu kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbyea pale ambapo walikuwa wakicheza.

Kimbe amesema baada ya kumaliza ziara hiyo timu inataraji kurudi Mbeya na kisha kuangalia mapendekezo ya benchi la ufundi chini ya kocha mkuu Juma Mwambusi kuona kama watacheza mipambano mingine nje ya Mbeya.

Amesema upo uwezekano wa kucheza michezo mingi ya kirafiki kulingana na maelekezo ya kocha huku akiweka hadharani kwamba mikoa ya nyanda za juu kusini itapatiwa fursa ya kutembelea na timu yao endapo kunatimu zitakazohitaji kucheza nao.

Aidha Katibu huyo amewataka mashabiki wa timu hiyo kote nchini kuendelea kuwaunga mkoano kwa asilimia mia moja kwani wamejiandaa kufanya vyema  msimu ujao wa ligi kuu ya soka Tanzania bara unaotaraji kuanza sept 20 mwaka huu.

Amebainisha kuwa mshikamano uliokuwepo msimu uliopita kati yao na mashabiki ndio ulisaidia wang'are hivyo na msimu huu unaokuja wazidi kuwaunga mkono na wao hawata waangusha.


   Kocha Juma Mwambusi akitoa maelekezo kwa vijana wake.

                             Kikosi cha Mbeya City.

Mkule.blogsport.com


No comments:

Post a Comment