Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 14, 2014

ANTONIO CONTE KOCHA MPYA WA TIMU YA TAIFA YA ITALIA.




                                                                                   Antonio Conte.


Shirikisho la soka nchini Italia maarufu kama  FIGC limemtangaza kocha wa zamani wa klabu ya Juventus Antonio Conte  kuwa vkocha mpya wa  timu ya taifa ya nchi hiyo .

Conte mwenye umri wa miaka 45 amechaguliwa na shirikisho hilo kurithi mikoba ya Cesare Prandelli aliyejiuzulu baada ya kuondoshwa mapema katika michuano ya kombe la dunia iliyomalizika mwezi julai nchini Brazil.

Shirikisho la soka nchini Italia  limethibitisha taarifa hiyo katika tovuti yake kuwa tayari Conte amesaini mkataba wa miaka miwili ya kukinoa kikosi hicho hadi mwaka 2016.

Kuchaguliwa kwa kocha Conte imekuja siku chache baada ya nchi ya Italia kumchagua Raisi mpya wa shirikisho hilo Carlo Tavecchio kurithi mikoba ya Giancarlo Abete alijiuzulu kutokana na nchi yake kushindwa kutwaa kombe la dunia msimu huu.

                                       Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment