Wakati kampeeni zikiendelea kwenye
uchaguzi wa chama cha soka mkoani Iringa (IRFA)mgombea wa nafasi ya ukatibu
mkuu Doct.Ally Ngara amesema endapo akifanikiwa kushinda kwenye uchaguzi huo ataleta
mapinduzi ya soka katika mkoa huo.
Ngara ambaye anakabiliwa na upinzani
kutoka kwa mgombe mwenzake Ramadhani Mahano amesema mara baada ya kuchaguliwa atafanya mambo mhimu ambayo yatakuwa dira
nzuri ya kuliendelezaoka la mkoa huo ambalo limepoteza mwelekeo kwa kiasi
kikubwa kwa hadi sasa ni zaidi ya miaka 10 mkoa huo hauna timu ya ligi kuu
baada ya Lipuli kushuka daraja miaka 13 iliyopita.
1.Kuhakikisha anarejesha mshikamano
miongoni mwa viongozi wa vyama vya soka katika vilaya za mkoa huo na ule wa
mkoa (IRFA)pamojana na wadau wa mchezo huo.
2.Kuvunja matabaka ambayo yapo kwakuwa uwepo wa matabaka utasababisha mpasuko ambao utafanya soka lisiiende kama ambavyo wadau wengi
wanahitaji.
3.Uongozi wake hautafumbia macho
masuala ya upangaji wa matokeo kwa vilabu vya soka mkoani humo kuanzia ngazi ya
chini hadi juu na kiongozi yeyote wa klabu au mchezaji atakaebainika kufanya
tabia hiyo atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
4.Kuhakikisha chama cha soka kinakuwa
na ofisi yake ambayo itashughulikia masuala ya mpira pekee na itakuwazi kwa
wanamichezo hususani mpira wa miguu kutoa mawazo yao,malalamiko yao ambayo
wanayo jambo litakalo saidia uongozi
wake kuwa na utendaji bora zaidi.
(Hadi sasa uongozi wa chama cha soka hauna ofisi maalumu
kwani hata katibu aliyepita alikuwa anatumia ofisi yake binafsi)
5.Kutii kiu ya wadau wa mpira wa miguu
mkoani Iringa ambao wanamapenzi makubwa na mchezo huo na sasa wanahitaji walau
kuona ligi kuu ikichezwa kwenye mkoa huo.Amesema mara baada ya kuchaguliwa
atahakkikisha anapandisha timu zote zilizopo ligi daraja la kwanza Lipuli fc na
Kurugenzi fc ya Mafinga kwenda ligi kuu na kama sio zote basi hata mmoja na
hilo litafanyika katika msimu wa kwanza atakaokuwa madarakani.Atahakikisha hilo
linafanikiwa kwakushirikiana na viongozi waliopo na wadau wote wenye kiu ya
kuona ligi kuu.
6.Kuwaheshimu na kuwathamini wale
wote watakaotoa mali zao mawazo yao ya
kuendeleza mpira wa miguu kwenye mkoa wa Iringa kwakuwa kufanya hivyo
hakutajenga hofu tena iliyopo kwa miongoni mwao ambao wameshapoteza imani na soka
la mkoa huo.
7.Kuwashirikisha wakongwe wote
waliowahi kucheza soka katika mkoa wa Iringa na wale wanaoijua vyema historia
ya soka la mkoa huo kwakuwa wao ndio wanaojua jinsi mchezaji anavyoumia
anapokuwa uwanjani.
Amesema atahakikisha Wakongwe hao
wanaheshiwa na kuthaminiwa huku wakishirikishwa katika mikutano mbalimbali ya
maendeleo ya soka la mkoa wa Iringa jambo ambalo halifanyiki sasa na badala
yake wanachukuliwa kama watu wa kawaida.
8.Kuanzisha ligi mbalimbali nyingi
zenye masharti nafuu ili kutoa nafasi ya vijana kucheza mpira.Amesema wapo
wadau mbalimbali ambao wamekuwa mstari wa mbele kuanzisha ligi au mashindano
mbalimbali ili kusaidia maendeleo ya soka la mkoa huo kwenda mbele.
9.Kusimamia soka la wanawake na
viongozi wa chama cha soka la wanawake waliopo
mkoani humo na atahakikisha kunakuwa na ligi mbalimbali za soka la
wanawake katika wilaya za mkoa huo.Amesema hilo litasaidia kukua kwa maendeleo
ya soka la wanawake mkoa wa Iringa.
10.Uhusiano kuwa mzuri baina ya
chama cha soka mkoani humo na vyama shiriki kama chama cha waamuzi,chama cha
madaktari,chama cha makocha,na vyama vingine vyote shiriki ili pale cha
chochote shiriki kinapokuwa na matatizo washirikiane kwa pamoja kutatua
changamoto zinazowakabili.
Amesema suala la kupata kocha yeyote
wa timu ya mkoa iwe ya vijana au wakubwa mchakato huo utashirikisha chama cha
makocha mkoa ili kusikiliza mawazo yao na kuona kocha yupi anayefaa.
Ngara amesema kero zote za waamuzi
zitashughulikiwa ili kurejesha heshima kwa waamuzi wa soka inayoonekana
kuporomoka kwa kiasi kikubwa na pia kuhaklikisha taaluma ya urefarii wa soka
inaanzia katika ngazi ya watoto wadogo.
Mkule.blogsport.com.
No comments:
Post a Comment