Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 10, 2014

BAADA YA KUTUA BARCA VERMAELEN ATOA YA MOYONI.




                                        Vermaelen akiwa Barcelona.

Baada ya kufikia makubaliano ya kujiunga na klabu ya Fc Barcelona akitokea Arsenal mlinzi Thomas Vermaelen amesema kuichezea timu hiyo kutamfanya  awe bora zaidi ya ilivyosasa.
Vermaelen ambaye amefaulu vipimo vya afya tayari kwakujiunga na miamba hao wa La liga kwa uhamisho wa Euro milioni 19 amesema kwake ni heshima kujiunga na timu hiyo kwani ndoto ya wachezaji wengi ni kucheza kwenye klabu kubwa.
Raia huyo wa Ubelgiji amesema ni jambo jema kwa yeye kujiunga na Barcelona kwasababu kama atafanya mazoezi kila siku na wachezaji wa timu hiyo atakuwa bora tofauti na alivyokuwa Arsenal.

                             Mlinzi mpya wa Fc Barcelona Thomas Vermaelen.

Vermaelen ambaye ni nahodha wa tatu kuihama Arsenal ndani ya miaka saba akiungana na Rubin Van Persie na Cesc Fabrigass amesema atajitahidi kuzoea mazingira mapya kwakuwa yupo kwenye nchi tofauti,lugha tofauti na utamaduni tofauti.

                            Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment