Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 28, 2014

ROONEY KATIKA MWAKA WA HESHIMA, APEWA UNAHODHA WA ENGLAND.




Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson  amemteua mshabuliaji wa Manchester United Wayne Rooney kuwa nahodha mpya  kuchukua nafasi hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na kiungo wa Liverpool Steven  Gerrard aliyestaafu mwezi uliopita.
Rooney mwenye umri wa miaka 28 ameshafunga magoli 40 kwenye timu ya taifa katika michezo 95 aliyocheza  hadi sasa na ataanza kuvaa kitamba cha unahodha kuanzia kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Uingereza na Norway septemba 3 mwaka huu.
Kocha  Roy Hodgson amesema anaamini Rooney anastahili kuwa nahodha wa Uingereza na kuteuliwa kwake kuwa nahodha wa Manchester United hivi karibuni kulidhihirisha kwamba anafaa kwa nafasi hiyo.
Aidha kocha huyo ametangaza kikosi kitakachocheza mchezo wa kirafiki mwezi ujao dhidi ya Norway kabla ya kuikabili Uswis Septemba 8 mwaka huu chenye makipa  Fraser Forster (Southampton), Ben Foster (West Bromwich Albion), na Joe Hart (Manchester City)
Walinzi ni Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Calum Chambers (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Phil Jones (Manchester United), Danny Rose (Tottenham Hotspur),na  John Stones (Everton)
Viungo ni Jack Colback (Newcastle United), Fabian Delph (Aston Villa), Jordan Henderson (Liverpool), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal) Raheem Sterling (Liverpool), Andros Townsend (Tottenham Hotspur), na Jack Wilshere (Arsenal)
Washambuliaji ni  Rickie Lambert (Liverpool), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), na Danny Welbeck (Manchester United)

                                          Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment