Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 9, 2014

BREAKING NEWSSSSSSSSSSSSSSSSSS MAN UNITED YATANGAZA NYOTA WANAOUZWA.




                                                         Louis Van Gaal.


Mabingwa mara 20 wa ligi kuu ya England Manchester United imeweka hadharani wachezaji wake inayowauza hivi sasa na kocha mkuu wa mashetani hao wekundu Lous Van Gaal ameitaka klabu yeyote inayowahitaji kuwasiliana na uongozi wa timu hiyo.
Majina ya nyota wanaouzwa yametangazwa siku 7 kabla ya kuanza kwa ligi kuu ya nchini England na ni sehemu ya tamko alilolitoa kocha Louis Van Gaal baada ya kurejea England wakitokea Marekan ambapo timu hiyo ilikuwa ikicheza michezo mbalimbali ya kirafiki na kufanya vyema kwa asilimia kubwa.
Van Gaal alitangaza kuwa baada ya kuwapa wachezaji wote 26 kucheza katika mechi za majaribio ameshajua uwezo wa mchezaji mmoja mmoja hivyo kumpa nafasi ya kuona ni nyota wapi hawatakuwa kwenye mipango yake.

Wafuatao kwenye picha ni wachezaji wanaouzwa na thamani zao.

                  1.Felain,2.Wilfred Zaha,3.Chicharito,4.Shinji Kagawa,5.Anderson.,6.Luis Nani.

Pamoja na hayo kocha huyo anatarjiwa kumtangaza nahodha mpya wakati wowote baada ya aliyekuwa akishikilia kitambaa cha unahodha Nemanja Vidic kuhamia Inter Milan ya Italia.
Wanaopendekezwa kuwa huenda mmoja wao akawa nahodha ni Robin Van Persie na Wayne Rooney.
                     
                                 Mkule.blogsport.com.

No comments:

Post a Comment