Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 31, 2014

ANDY MURRY ASEMA YUPO FITI KUMKABILI JO-WILFRED TSONG US OPEN 2014.



                                       Andy Murry.

Wakati akijiandaa kumkabili Jo-Wilfred Tsonga katika  michuano ya wazi ya Marekani mcheza tenisi Andy Murry amesema anaamini atafanya vyema licha ya kusumbuliwa na maumivu kwa siku kadhaa hivi sasa.
Murry ambaye amefanikiwa kuingia mzunguko wanne wa mashindano hayo baada ya kumshinda Andrey Kuznetsov jana jumamosi kwa seti 6 kwa1,7 kwa 5,4 kwa 6 na 6 kwa 2 amesema ushindi huo umedhihirisha kwamba amepona vyema.
Akizungumza baada ya ushindi huo Murry anayeshika nafasi ya 9 kwa ubora wa mchezo huo duniani upande wa wanaume amebainisha kwamba uwezo aliouonesha hapo jana ulikuwa ni wa hali ya juu lakini akiahidi kuongeza kasi zaidi.
Michuano hiyo ya wazi imeingia katika wiki ya pili ambapo wachezaji mbalimbali wa kiume na wakakike duniani wanapambana nchini Marekani kuwania ubingwa kwa mwaka huu.

                              Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment