Monday, August 25, 2014
KUFUATIA KIFO CHA MCHEZAJI,SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI ALGERIA LASIMAMISHA MICHEZO YA LIGI MWISHONI MWA JUMA HILI.
Marehemu Albert Ebosse enzi za uhai wake.
Shirikishoa la soka nchini Algeria FAF limesimamisha michezo yote ya ligi daraja la kwanza iliyokuwa ichezwe mwishoni mwa juma hili kufuatia kifo cha mchezaji Albert Ebosse kilichotokea jana kwakupigwa na kitu kigumu akiwa uwanjani.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alifariki mwishoni mwa mchezo baina ya timu yake ya JS Kabylie na USM Alger uliomalizika kwa JS Kabylie kufungwa magoli 2 kwa1 huku goli pekee la timu hiyo likiwa limefungwa na marehemu Albert Ebosse's.
Taarifa ya shirikisho hilo imesema kuwa michezo yote iliyokuwa ichezwe tarehe 29 na 30 ya mwezi huu haitokuwepo hadi itakapotangazwa hapo baadae mara pindi uchunguzi wa tukio hilo kukamilika na hatua zaidi kuchukuliwa.
Tayari raisi wa shirikisho la soka barani Afrika Caf Issa Hayatou amewapigia simu viongozi wa shirikisho la soka nchini Algeria akiwataka kuchukua hatua kali kwa ukatili huo uliofanywa na mashabiki wahuni na CAF haitokuwa tayari kuvumilia uovu huo viwanjani.
Marehemu Albert Ebosse enzi za uhai wake.
Mkule.blogsport.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment