Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 6, 2014

KOCHA WA CHILE KUENDELEA NA KIBARUA CHAKE HADI MWAKA 2018.






Kocha wa timu ya taifa ya Chile Jorge Sampaoli amefikia makubaliano na shikrikisho la soka nchini humo ANFP kuendelea na kazi yake ya kukifundisha kikosi hicho hadi mwaka 2018 kwenye fainali za kombe la dunia zitakazofanyika Urusi.

Sampaoli mwenye umri wa miaka 54 jana alikuwa na mazungumzo na rais wa shirikisho la soka la Chile Sergio Jadue waliofikia makubaliano hayo baada ya kocha huyo kufanya vyema akiwa na timu yao ya taifa kwenye fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.

Tovuti ya shirikisho la soka la nchini Chile imethibitisha makubaliano hayo na Sampaoli ambaye aliiongoza timu yake hadi kwenye hatua ya 16 bora   kwenye kombe la dunia  mwaka huu na kutolewa na wenyeji Brazil kwa mikwaju ya penalti.

Sampaoli  ambaye ni raia wa Argentina alianza kuifundisha  timu ya taifa ya Chile mwaka 2012.

                                 Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment