Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 6, 2014

REINA KUTIMKIA BAYERN MUNICH.




                                                                       Pepe Reina.

Mabingwa wa ligi kuu ya Ujerumani timu ya Bayern munich imefikia makubaliano na mlinda mlango wa Liverpool  Pepe Reina kwaajili ya kumsajili kama msaidizi wa mlinda mlango namba moja Manuel Neuer.

Mwenyekiti wa Bayern Munich  Karl-Heinz Rummenigge amesema Reina ambaye msimu uliopita aliichezea Napoli ya Italia kwa mkopo anatarji kuwasili mjini Munich siku chache kutoka sasa kwaajili ya kufanyiwa vipimo na kusaini mkataba.

Pamoja na kukiri vilabu hivyo kufikia makubaliano ya kuuziana mchezaji huyo ambaye mwishoni mwa mwezi huu atafikisha miaka 32 wao kama Bayern Munich wameamua kumsajili Reina kwakuwa wanaamini atawasaidia.

Reina ambaye alikuwa mlinda mlango namba mmoja wa Liverpool kwa misimu minane nafasi yake ilianza kuonekana finyu kwenye kikosi cha timu hiyo baada ya kocha Brendan Rogers kumsajili mlinda mlango wa Ubelgiji Simon Mignolet kutoka Sunderland msimu uliopita.

                                   Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment