Nyota wa KCCA ya Uganda akiwa dimbani.
Hekaheka za michuano ya klabu bingwa
Afrika mashariki na kati maarufu kama Kagame intaraji kuendelea leo ambapo
michezo miwili ya nusu fainali inatarajiwa kuchezwa mjini Kigali Rwanda uwanja
wa Amahoro.
Katika nusu fainali ya awali Polisi
na APR zote za nchini Rwanda zitachuana vikali kuwania kufuzu fainali baada ya
timu hizo kufuzu hatua hiyo kwa kushinda michezo yao ya robo fainali,ambapo APR
iliifunga Rayon Sports na Polisi kuifunga Atletico ya Burundi.
Nusu fainali yapili itakuwa baina ya
wababe wa Azam fc timu ya Elmerekh ya Sudan dhidi ya KCCA ya Uganda ambayo
iliifunga Atlabara juba ya sudani kusini magoli 3 kwa 1 kwenye hatua ya robo
fainali.
Baada ya michezo ya leo fainali ya
michuano hiyo inayodhaminiwa na rais wa Rwanda Paul Kagame inataraji kuchezwa tarehe
24 kwenye uwanja wa Amahoro sambamba na pambano la kusaka mshindi wa tatu.
Polisi fc ya Rwanda itakayokwaana na APR nusu fainali ya michuano ya Kagame mjini Kigali.
Kikosi cha APR kitakachoivaa Polisi zote za Rwanda katika nusu fainali ya Kagame.
cha timu ya KCCA cha nchini Uganda kitakachoikabili El Merekh ya Sudani kwenye nusu fainali ya michuano ya Kagame leo mjini Kagali.
Kikosi cha timu ya El Merekh kitakachokabiliana na KCCA ya Uganda kwenye nusu fainali ya michuano ya Kagame mjini Kigali Rwanda leo.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment