Pages

Ads 468x60px

Monday, August 18, 2014

DZECO MBIONI KUSAINI MKATABA MPYA WA KUENDELEA KUBAKI MAN CITY.




                                                                           Edin Dzeco.
Kocha wa mabingwa wa ligi kuu ya England Manchester City  Manuel Pellegrin amethibitisha kuwa mshambuliaji Edin Dzeco anajiandaa kurefusha mkataba wake aendelee kubakia katika  timu hiyo.
Pellegrin amesema sababu za kumpatia mkataba mpya mchezaji huyo raia wa Bosnia kunatokana na uzwezo mzuri aliounyesha msimu uliopita nakusaidia  Manchester City kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England kwa mara ya pili katika historia.
Pelegrin amemsifia Dzeco aliyesajiliwa na kocha wa zamani wa timu hiyo Roberto Mancin kwa ada ya paundi milioni 27 akitokea Wolfsburg  mwaka 2011 kwakusema ni mchezaji mhimu ambaye anastahili kuendelea kubaki Manchester City.
Katika michezo 109 aliyocheza kwenye ligi kuu ya England Dzeco amefunga magoli 46 licha ya mara kadhaa kupata muda mfupi wa kucheza kutokana na ushindani wa namba katika kikosi hicho.

                            Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment