Pages

Ads 468x60px

Wednesday, November 13, 2013

IBRA KADABRA AWAPONDA WANAODHANI MECHI YA KESHO KATI YA SWEDEN NA URENO NI YA YEYE NA RONALDO.




Nahodha wa timu ya taifa ya Sweden na  PSG ya Ufaransa Zlatan Ibrahimovic amepinga mitazamo ya wachambuzi wa soka kuwa mchezo wa kesho baina ya timu yake ya taifa na Ureno  utakuwa ni kumshindanisha yeye na  Cristiano Ronaldo.
Zlatan amesema mchezo huo  unawakutanisha wachezaji wengi kutoka mataifa mawili kila mmoja akiiwakilisha nchi yake  hivyo wale wanaodhani utawakutanisha yeye na Ronaldo  hawako sahihi.
Raia huyo wa Sweden ambaye amekuwa  msaada mkubwa kwa taifa lake na klabu yake amebainisha  umhimu wa mchezo  huo ni kuwakutanisha wacheza wengi wazuri   na hilo ndilo jambo ambalo umma unapaswa kujua.
Sweden na Ureno zinacheza kesho mchezo maalumu wa kufuzu fainali zijazo za kombe la dunia  na baada ya hapo mataifa hayo yatarudiana  tarehe 19 ya mwezi huu mshindi atakayepatikana atakuwa amekata tiketi ya kwenda Brazil mwakani.

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment