Pages

Ads 468x60px

Saturday, November 9, 2013

WANAUME,NIGERIA U-17 ILIVYOTWAA UBINGWA WA KOMBE LA DUNIA HUKO FALME ZA KIARABU.




Timu ya Taifa ya vijana ya Nigeria chini ya miaka 17 imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya kombe la dunia huko umoja wa falme za kiarabu kwa kuifunga timu ya taifa ya Mexico kwa magoli 3-0.

Nigeria inayofundishwa na kocha Manu Garba imepata magoli hayo kupitia kwa Erick Aguirre aliyejifunga, mshambuliaji Kelechi Iheanacho na nahodha Mussa Muhammed.

Mexico ambao ndio walikuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo wameshindwa kulitetea taji hilo na kuwapa Nigeria ubingwa wa nne baada ya kufanya hivyo mwaka 1985, 1993 na 2007 ikiwa ni rekodi ya dunia.

Wakati huohuo Nigeria imevunjaa rekodi ya magoli katika michuano hio iliyowekwa mwaka 2011 na timu ya taifa ya Ujerumani kwa kufunga magoli 26.

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment