Pages

Ads 468x60px

Sunday, November 10, 2013

HATUJAACHANA NA KOCHA WETU YASEMA YANGA.





Uongozi wa mabingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga umekanusha taarifa za kumsainisha mkataba aliyekuwa kocha wa Azam fc  Stewart Hall na kumfuta kazi kocha wao  Arne Brandts kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vilivyoarifu.
Msemaji wa Yanga Baraka kizunguto amesema kuwa kocha mkuu wa Yanga  Arne Brandts ameenda mapumziko na anatarji kurudi nchini tarehe 24 ya mwezi huu kwaajili ya kuanza mazoezi ya kujiandaa na   duru ya pili ya ligi kuu.
Kizunguto amesema  hata suala la Yanga kumsajili Juma Kaseja ni mapendekezo yake na pia juu usajili mwingine wa kikosi hicho utakuwa ukilenga mapendekezo ya wachezaji ambao anawahitaji.
Aidha msemaji huyo amesema hawajafanya mazungumzo yeyote na aliyekuwa kocha wa Azam fc Stewart Hall kama ambayoimeripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari  huku akitoa ushauri wa bure kwa wanahabari kuandika habari za ukweli na sio kuidangavya jamii.
Hivi karibuni kumekuwa na uvumi kwamba Yanga imeachana na kocha wake na ipo kwenye mipango ya kumsainisha mkataba Stewart Hall ambaye ameifundisha Azam kwa mafanikio makubwa na sasa amekatisha mkataba wa kuifundisha timu hiyo.

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment