Pages

Ads 468x60px

Saturday, November 9, 2013

MTAZAMO WANGU JUU YA UJIO WA KASEJA NDANI YA YANGA BAADA YA KUSAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI NA MABINGWA HAO WA LIGI KUU TANZANIA BARA.




Mlinda mlango  aliyetemwa na Simba kisha kukaa miezi kadhaa bila timu Juma Kaseja amesaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara klabu ya Yanga yenye makao makuu yake jijini Dare-salaam.
Kaseja  ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa magolikipa bora kuwahi kutokea nchini  baada ya Mohamedi Mwameja “TANZANIA ONE” na wengineo ninavyoona mimi  ni kwamba uamuzi wa Yanga kusajili  Kaseja unasura kuu mbili ama tatu kwa wanaolijua vyema soka la Tanzania na vibweka vyake.
1.Kuisaidia Yanga ambayo imefanikiwa kumaliza duru ya kwanza  ya VPL licha ya kuanza vibara msimu huu.
Naamini Kaseja ni mchezaji ambaye Simba walifanya  kosa kubwa kumtema  wakati wakijua kabisa nyota huyo ambaye  anarekodi nzuri ya kuichezea timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars michezo mingi tangu aanze kuitwa miaka  aliachwa kwa  chuki za watu wa chache wenye sauti ndani ya Simba.Kitendo cha kuachwa na Simba kilimsikitisha kila mpenzi wa Simba ama shabiki wa timu hiyo lakini kwakuwa wao ni waongeaji wa magengeni haikusaidia Kaseja arudi tena msimbazi.
Kuona hivyo  macho na masikio yangu yalibaki yakisubiri kuona dhahabu hii ni nani wa kuiokota  au hapa naomba nitumie neon Mvinyo huu ni nani wa kuununua anayehitaji kupata ladha nzuri na yakipekee.Sikushangazwa na uamuzi wa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania taifa Stars Kim Poulsen kutomwita kwenye kikosi kinachojiandaa na michuano ya Challenge  naamini alifanya hivyo kiprofesheno.
Wenzetu Ulaya usipocheza kwenye kikosi cha kwanza kwenye klabu yako unahatihati ya kutoichezea timu ya taifa lako hii tumeiona kwa wachezaji wengi  kama Demba Ba ambaye ameshindwa kuitwa kwenye kikosi cha Senegal licha ya kuwa ni mzuri na kutokuwa chaguo la kwanza ndani ya klabu yake ya Chelsea mambo yamekuwa hivyo.
Nirudi kwa kaseja,Naamini Yanga imelamba dume kwakumpata Kaseja  na sintoshangaa tena kuona anakuwa golikipa namba moja na kuwaacha midomo wazi waliomkejeli na kumuona hafai.Kweli ukikiona cha nini wenzio wanajiuliza watakipata lini,hatimae Yanga wanakila sababu ya kujivunia kumpata Kaseja.
Miaka miwili aliyosaibni Yanga Kaseja  ataendelea kuijenga heshima yake kwakuwa najua  atakuwa na Yanga katika michuano ya klabu bingwa Afrika na  atawasaidia wakimtumia vyema.
Angalizo langu ni kwa wale wenye imani  za kishirikina kwamba ukiona mtu flani amewekwa benchi unahoji nakuingiza imani za kishirikina kwamba si unaona si unaona,tuachane na imani hizo haiwezekani kocha akamweka benchi mchezaji mwenye nidhamu na uwezo mzuri mambo ambayo binafsi naamini huwasaidia wachezaji wengi duniani.
Sikushangaa kuona Casilas akikalishwa benchi na Mourinho ndani ya Ral Madrid kwa mooja ya sababu nilizozitaja hapo juu hivyo sintoshangaa kuona Kaseja  akiwekwa benchi  Yanga ka uwezo wake utashuka au akimweka mtu benchi endapo ataonekana ni bora zaidi yao.
Usikose kufuatilia sababu zingine  ambazo naamini kwanini Yanga imeamua kumsajili Juma Kaseja. 

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment