Pages

Ads 468x60px

Friday, November 8, 2013

MANCHESTER CITY YAPATA PIGO,DAVID SILVA KUKAA NJE YA UWANJA MWEZI MMOJA KWA KUSUBULIWA NA JERAHA LA MGUU.





Kiungo mchezeshaji wa klabu ya Manchester City ya nchini England David Silva anataraji kukaa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja  kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli  kwenye kigimbi cha mguu.
Raia huyo wa Hispania  anakadiriwa kuwa atakosa michezo mitano ya klabu yake huku akitarajiwa kurudi dimbani tarehe saba ya mwezi ujao ambapo Manchester City itakuwa ikicheza na Southampton katika ligi kuu ya England.
Silva  mwenye umri wa miaka 27 amefunga magoli 3 katika michezo 7 ya ligi kuu ya nchini England.
Pamoja na kumkosa David Silva kwenye michezo ya hivi karibuni kocha wa timu hiyo Manuel Pellegrin anamatumani makubwa  kwamba nahodha Vicent Kompany atakuwepo katika mchezo baina yao na Tottenham hotspurs nov 24 baada ya kukaa nje ya uwanja  tangu mwanzoni mwa mwezi uliopita akisumbuliwa na maumivu ya  nyama za paja.

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment