Pages

Ads 468x60px

Tuesday, November 26, 2013

LICHA YA KUIPA TANO ARSENAL GIGGS ASEMA MANCHESTER UNITED ITATEA UBINGWA WA BPL MSIMU HUU.




Mkongwe wa Manchester United  Ryan Giggs  amesema kikosi cha Arsenal kinastahili kuongooza ligi hadi hivi sasa lakini akisistiza kuwa United bado wanauwezo mkubwa wa kushinda taji la ligi kuu ya nchini England kwa mara ya 21.
Arsenal ambayo inaongoza ligi kwa alama 28 ikiwa ni tofauti ya alama 4 na timu inayoifuatia huku Manchester United ikihitaji alama 9 kukaa juu yake bado Gigis anamatumaini makubwa ya kutetea ubingwa wao msimu huu wa 2013/2014.
Giggis amekiri kuwa matokeo mabaya waliyoyapata kwenye michezo 10 ya mwanzo wa ligi ndiyo yaliyosababisha kufika hapo walipo hivi sasa huku akiongeza kuwa kila mchezaji wa Man United hajafurahishwa na michezo waliyocheza hadi sasa.
Manchester United ambayo mchezo wake unaofuata katika ligi kuu ya England inakutana na Tottenham Hotspurs bado  Giggis anamaani  kikosi chao kitarudi kwenye ubora uliozoelka kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wa 2013.

mkule.blogspot.com
 

No comments:

Post a Comment