Pages

Ads 468x60px

Tuesday, November 19, 2013

STARS YALAZIMISHWA SARE YA KUTOFUNGANA NA WAZIMBABWE UWANJA WA TAIFA.



Timu ya soka ya taifa ya Tanzania taifa stars leo imelazimishwa sare ya kutofungana na timu ya taifa ya Zimbabwe kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa kunako dimba la taifa jijini Daresalaam.
Katika mchezo huo stars licha ya kuwa na kikosi chake kamili imeshindwa kufurukuta mbele ya Zimbabwe na kujikuta ikitolewa jasho na wapinzania wao.
 Pamoja na kuwa mbele ya ashabiki wake walishindwa kupata walau goli mmoja japo walipata nafasi kadhaa za kufunga lakini hadi dakika 90 zinamalizika Stars 0 Zimbabwe 0.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Ivo Mapunda, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni/Himid Mao dk56, Aggrey Morris, Kevin Yondan, Frank Domayo, Hassan Dilunga/Salum Abubakar dk51, Mwinyi Kazimoto/Amri Kiemba dk51, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Mrisho Ngassa/Farid Mussa dk80.

Zimbabwe; Tapiwa Kapini, Ocean Mushere, Carrington Nyandemba, Obey Mureneheri/Misheck Mborai dk46, Themba Ndhlovu/Felix Chidungwe, Isaac Majari/Patson Jaure, Kapinda Wonder, Kundawashe Mahachi, Warren Dube/Nkosana Siwela, Lot Chiungwa/Gerald Ndhlovu na Simba Sithole. 


Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment