Pages

Ads 468x60px

Thursday, November 21, 2013

AGUERO AIZODOA REAL MADRID ASEMA KAMWE HANA MPANGO WA KUJIUNGA NAYO.




Mshambuliaji wa timu ya Manchester City inayoshiriki ligi kuu ya nchini England Sergio Aguero  amekanusha vikali taarifa zilizovuja kuwa amefikia makubaliano na Real Madrid kwaajili ya kujiunga nayo mwezi januari mwakani.
Raia huyo wa Argentina ambaye amekuwa msaada mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji ya kikosi cha City  pia ameinyooshea kidole Real Madrid  akisema kamwe hana mpango wa kujiunga  nao.
Aguero maarufu kama “Kuni” amebainisha kuwa ukweli ni kwamba anajisikia furaha na  maisha ya Manchester  na anahudumiwa vizuri na timu tofauti na akiwa Hispania au Argentina taifa alilozaliwa.
Aguero alijiunga na Manchester City akitokea Atletico Madrid mwaka 2011 kwa uhamisho wa paundi milioni 35 na kwasasa amekuwa kwenye kiwango kizuri chini ya kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini.


                     Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment