Shirikisho la soka la Ghana G.F.A limeendelea kuomba ulinzi zaidi kwa
nchini ya Misri juu ya timu yao ya taifa itakapocheza mchezo wa marudiano
kufuzu fainali za mwakani za kombe la
dunia baina ya mataifa hayo mawili.
Ujumbe
wa watu wanne kutoka shirikisho
la soka nchini Ghana jana umewasili
nchini Misri kwaajili ya kufanya mazungumzo ya pamoja ya kuimarisha usalama
kwenye mchezo huo unaotaraji kuchezwa juma lijalo.
Mjumbe wa bodi ya shirikisho la soka nchini
Misri Ehab Laheita aliyehudhuria kikao hicho amethibitisha kufanyika kwa
mazungumzo nakusema ujumbe wa Ghana umeomba timu yao na mashabiki wake kupatiwa
ulinzi zaidi.
Ujumbe wa Ghana umeongozwa na rais wa
shirikisho la soka nchini humo Kwesi Nyantakyi,Abedi Ayew Pele,Alhaji Saeed
Lartey ambaye ni afisa usalama wa taifa
hilo pamoja na msemaji wa F.A ya Ghana
Ibrahim Sannie.
Posted by Yusuph Mkule.
No comments:
Post a Comment