Pages

Ads 468x60px

Monday, November 18, 2013

HUYU NDIYE KOCHA MPYA WA TIMU YA TAIFA YA JAMHURI YA IRELAND ATAKEANZA KIBARUA CHAKE JANUARI 2014.



Kocha wa klabu ya Victoria Pilsen Pavel Vrba anatarajiwa kuanza kuifundisha timu ya taifa ya Jamhuri ya Czech mwezi januari mwakani  baada ya shirikisho la soka nchini humo FACR kuthibitisha kwa kutoa tangazo.
Rais wa shirikisho hilo Miroslav Pelta amebainisha kuwa  kazi kubwa ya Pavel Vrba itakuwa  ni kuanza kuiandaa timu yao kwaajili ya michezo ya mchujo wa kombe la mataifa ya Ulaya  2016 na mkataba wake utaenda hadi mwezi juni  mwaka 2015.
Kwaupande wao uongozi wa Victoria Pilsen umesema kuwa wamekubaliana na uamuzi wa Vrba ambaye ameona ni vyema kutafuta changamoto mpya za maisha  na ataondoka tarehe 15 mwezi ujao.
Tangu awasili kwenye timu ya Victoria Pilsen mwaka 2008  Vrba ameshinda mataji mawili  ya ligi na kuiwezesha kucheza michuano ya klabu bingwa Ulaya  ikiwemo na msimu huu.

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment