Pages

Ads 468x60px

Wednesday, November 27, 2013

ZANZIBAR HEROES YAANZA VYEMA MICHUANO YA CHALLANGE NCHINI KENYA YAICHAPA SUDANI KUSINI 2-1.







Timu ya taifa ya Zanzibar Zanziba Heros imeanza vyema mashindano ya kombe la Challenge yaliyoanza leo nchini Kenya baada ya kuifunga Sudani kusini magoli 2 kwa 1.

Mchezo huo  wa kwanza  wa mashindano hayo yanayoshirikisha nchini wanachama wa Cecafa magoli ya Zanzibar heros  kwenye pambano hilo lililohudhudhuriwa na watazamaji wachache yamefungwa na Suleiman Kassim ‘Selembe’  dkk 7 huku lile la pili likifungwa na Adeyoum Saleh Ahmed katika dkk 67.

Bao la kufutia machozi kwa Sudani kusini limepatikana dkk 73 likifungwa na Fabiano Lako.
Kikosi cha Zanzibar kilikuwa kama ifuatavyo;- Abdallah Rashid, Salum Khamis/Ally Khan dk78, Waziri Salum, Shaffi Hassan, Mohamed Fakhi, Sabri Ali, Masoud Ali, Suleiman Kassim, Awadh Juma na Khamis Mcha/Amour Omar dk44/Adeyoum Saleh dk62. 

kikosi cha Sudan Kusini kilikuwa kikiongozwa na ;- Juma Jinaro, Atar Thomas, Philip Delfino, Edomon Amadeo, Richard Justin, Wiiam Offiri, Jimmy Erasto, Thomas Jacob, Godfrey Peter, Francis Khamis/Fabiano Lako dk68 na James Joseph. 

mkule.blogspot.com

No comments:

Post a Comment