Pages

Ads 468x60px

Thursday, November 21, 2013

ZFA YAPOKEA MSAADA WA T.SH MILIONI TANO KWAAJILI YA MAANDALIZI YA ZANZIBAR HERO'S.



Chama cha soka visiwani Zanzibar ZFA kimepokea msaada wa shilingi million tano ambazo zimetolewa na bodi ya ligi kwa ajili ya kusaidia maandalizi ya timu ya taifa ya Zanzibar  Zanzibar Heroes ambayo itashiriki michuano ya kombe la challenge iliyopangwa kufanyika nchini Kenya mwishoni mwa mwezi huu.
 Afisa mtendaji wa bodi ya ligi Sailas Mwakibinga amesema wametoa fedha hizo kwa ZFA zenye lengo la kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo kati ya chama hicho na shirikisho la soka nchini Tff  pamoja na bodi hiyo.
Ameongeza kuwa milango ipo wazi kwa ZFA kushirikana na shirikisho la soka nchini ili kuimarisha mahusiano ya pande hizo mbili na anamatumaini kuwa uhusiano huo utaimarika zaidi ya kwa manufaa ya taifa.
Wakati huo huo katibu mkuu wa chama cha soka visiwani Zanzibar ZFA Salum Hadji Kassim amesema suala la kuachwa kikosini kwa wachezaji  Agrey Moris  na Nadir Haroub Ally Canavaro halina uhusiano wowote na adhabu walizozitangaza baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la Challenge mwaka jana nchini Uganda.
Ameongeza kuwa suala la kuachwa kwa mchezaji ni uamuzi wa benchi la ufundi kwakuwa  ndilo linalochagua timu ya taifa.

                            Posted by Yusuph Mkule. 


 Uongozi wa timu ya Ashanti Utd umekanusha taarifa za kuwasimamisha baadhi ya wachezaji kwamadai ya kuchukua rushwa wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Simba ambao walichomoza na ushindi wa mabao 4 kwa 2.
Msemaji Ashanti Utd Rajab Marijan amesema wanashangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuvumisha taarifa za kusimamishwa kwa wachezaji wao  nakuongeza kuwa uongozi ndio wenye mamlaka ya kutoa taarifa zote za klabu.
Amesema hakuna mchezaji awa wachezaji ambao wamesimamishwa kwa tuhuma za kupokea rushwa na wachezaji wao wote wapo tayari kwaajili ya duru ya mwisho ya ligi kuu ya soka Tanzania.
Aidha Marijan amekanusha taarifa zingine ambazo zinawahusisha baadhi ya viongozi wa timu yao  ambao wanadaiwa walihusika katika kuuza mchezo wao dhidi ya Simba kwakusema hakuna jambo kama hilo ambalo limezungumzwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini. 

 Posted by Yusuph Mkule.



 KAMATI YA UTENDAJI YA CHAMA CHA MPIRA MKOA WA RUVUMA KUKUTANA LEO.
Kamati ya utendaji ya chama cha mpira mkoa wa Ruvuma "FARU" leo inakutana kwaajili ya kujadili masuala mbalimbali ikiwemo ligi ya mkoa huo.
Mwenyekiti wa chama hicho Golden Sanga amesema mmoja ya ajenda itakauwa kujadili ligi ya mkoa ambayo inataanza mara baada ya wilaya zote za mkoa huo  kumaliza ligi zao.
Amesema kikao hicho kinatarajikutoa na tarehe ya kuanza kwa ligi hiyo  ambapo hadi hivi sasa bado muda wa timu kuchukua fomu za ushiriki unaendelea baada ya kusogeza mbele mchakato huo kutoka noveba 11 iliyokuwa siku ya mwisho
Aidha Sanga amezungumzia suala la ukarabati wa uwanja wa majimaji ambapo tayari wameshaanza hatua za awali na wanataraji kukutana na wamiliki wa uwanja huo unaotumiwa na vilabu vya majimaji na Jkt Mlale.
Amesema kamati maalumu itakayokutana na wamiliki wa uwanja huo itakuwa chini ya uenyekiti wake na wanaimani mchakato huo utazaa matunda na wadau wa  Ruvuma wasiwe na wasiwasi wa kutazama michezo ya ligi kwa timu zao kwakuwa itachezwa kwenye dimba la majimaji.

Posted by Yusuph Mkule.


  KIBADENI ALONGA BAADA YA KUTIMULIWA SIMBA.
Baada ya kutupiwa virago na Simba aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi hicho Abdalaah King Kibadeni hajapata barua yeyeote ya kufukuzwa na taarifa hizo anazisikia kwenye vyombo vya habari pekeee.
Kibadeni mbali na kuonyesha kusikitishwa kwake na njia ya kuachishwa kazi Simba amelaani kitendo cha baadhi ya vyombo vya habari kutafsiri kufukuzwa kwake wakifananisha na kupewa talaka akisema ni kauli za uzalilishaji.
Amesema alitegemea busara zilizotumika kumleta samba kutoka Kagera Sukari timu aliyokuwa akiifundisha ndizo zingetumika na si kama walivyo mfanyia.
Hata hivyo kocha huyo aliyewahi kuichezea Simba kwa mafanikio makubwa amewakosoa waliowaengua yeye na benchi lake la ufundi kwa kutotumia busara kwakutowapatia burua ya kuvunja mikataba yao.

           Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment