Pages

Ads 468x60px

Saturday, November 23, 2013

HAUZWIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII, MOURINHO AZIONYA REAL MADRID NA FC BARCELONA.





Kocha mkuu wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amesistiza kuwa  nyota wa timu hiyo raia wa Brazil Ramires hauzwi kwa bei yeyote mwezi januari mwakani wakati wa dirisha dogo la usajili barani Ulaya.
Ramires mwenye umri wa miaka 26  kwa majuma kadhaa yaliyopita amekuwa akiwindwa na  vilabu vya Real Madrid na mabingwa wa La liga klabu ya Fc Barcelona lakini kauli ya Mourinho  inamaanisha  ndoto za vilabu hivyo kumsajili mbrazil huyo zitakuwa zimeota mbawa.
Aidha Mourinho ameongeza kuwa mchezaji Thibaut Courtois naye hatouzwa kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vinavyoarifu kwamba mchezaji huyo anayeidakia Atletico Madrid kwa mkopo  atajiunga na timu hiyo kwa  mkataba wa kudumu.

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment