Pages

Ads 468x60px

Saturday, November 16, 2013

NIGERIA YAFUZU FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA MWAKANI HUKO NCHINI BRAZIL.


Timu ya soka ya taifa  ya Nigeria  imekuwa taifa la kwanza barani Afrika kufuzu fainali zijazo za kombe la dunia baada ya kuifunga Ethiopia magoli 2 kwa 0 pambano lililochezwa kwenye uwanja wa U.J. Usuene mjini Calabar nchini Nigeria.

katika mchezo huo magoli ya Nigeria yamefungwa na wachezaji Victor Moses kwa mkwaju wa penalti dakika ya 20 kabla ya Victor Obinna dakika ya 82 kufunga bao la pili na kuihakikishia Nigeria ambao ni mabingwa wa Afrika kupata tiketi ya kwenda Brazil mwakani.

usiku huu kuna mchezo mwengine wa kufuzu fainali hizo kwa nchi za Afrika  baina ya simba wa terana Senegal na Ivory Coast.

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment