Pages

Ads 468x60px

Friday, November 22, 2013

RT YAPOKEA MSAADA WA SHILINGI MILIONI TATU ZA KITANZANIA.




Shirikisho la riadha nchini RT limepokea hundi ya shilingi milioni 3 kutoka toka mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii(NSSF) mkoa wa Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya riadha yanayoratajia kufanyika mwakani.

Kaimu meneja wa NSSF mkoa wa Morogoro Mrisho Mwisimba amesema mfuko huo umetoa kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za kuendelea mchezo huo.

Raisi wa shirikisho la riadha nchini  Anthon Mtaka mara baada ya kupokea hundi hiyo  amesema kuna haja kwa wanamichezo kujiunga na mifuko ya jamii kwa ajili ya kuwasaidia pale wanapostaafu.

Aidha Mtaka amewakumbusha wanamichezo kujiunga na mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamiii ili kunufaika baadae.

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment