Pages

Ads 468x60px

Wednesday, November 13, 2013

YOUNG FUTURE TAIFA STARS YAWAADHIRI KAKA ZAO "TAIFA STARS" YAWANYUKA 1-0.




TIMU ya soka  Future Young Taifa Stars jioni ya leo  imeifunga timu ya kwanza taifa , Taifa Stars goli  1-0 katika mchezo maalum wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Goli  pekee la vijana hao  limefungwa na mshambuliaji wa Ruvu Shooting ya  mkoani Pwani, Elias Maguri aliyeunganisha mpira krosi kutoka kwa kinda wa  Mtibwa Sugar ya Morogoro, Juma Luizio ambaye  alimpokonya mpira mlinzi wa Yanga Kevin Yondan.

Katika mchezo huo  Future young taifa Stars imeonyesha kandanda safi na la kuvutia.

Kipa Ivo Mapunda wa Gor Mahia ya Kenya alipewa nafasi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Barthez lango la Stars na akadaka dakika 45 zote bila kuruhusu bao licha ya Future taifa stars kushambulia kwa wingi.
Baada ya mechi, kocha wa Stars, Kim Poulsen ameeleza kuvutiwa kwake na  uwezo wa mlindamlango Ivo  Mapunda na kwa ujumla mechi hiyo imemsaidia katika mkakati wake wa kuunda kikosi imara cha kudumu.
Rais mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi alikuwepo Uwanja wa Karume na baada ya mechi alizungumza na wachezaji akiwataka wafanye kazi nzuri ili wafurahie matunda ya uongozi wake.
Aidha Malinzi amewaambia wachezaji wa Stars kuwa Novemba 19 watacheza na Kenya, Harambee Stars, mchezo wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.  



Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment