Pages

Ads 468x60px

Thursday, November 14, 2013

GUS-POYET APATA RUHUSA YA KUSAJILI NYOTA WATANO KUKIONGEZA NGUVU KIKOSI CHA SUNDERLAND MWEZI JANUARY.



Kocha wa timu ya  Sunderland inayoshiriki ligi kuu ya England Gus Poyet amepewa ruhusa na uongozi wa klabu hiyo  kusajili wachezaji  mwezi wa kwanza mwakani ili kuimarisha kikosi hicho.
Poyet ambaye alichukua nafasi ya Paolo Di Canio  anampango wa kusajili wachezaji watano mhimu watakaosaidiana na waliyopo ili kuipa nguvu timu hiyo inayoshika nafasi ya kumi na tisa katika msimamo wa ligi kuu ya England msimu huu.
Timu hiyo maarufu kama paka weusi inahitajika kushinda michezo mitatu ili iukimbie mstari wa kushuka daraja  kutokana na kuwa  na alama saba pekee huku ikishinda michezo miwili kati ya kumi na mmoja iliyocheza.
Katika mchezo wake wa hivi karibuni timu hiyo iliifunga  Manchester City goli 1 kwa 0   na  juma lijalo inakabiliwa na mchezo dhidi ya Stock City kabla ya kucheza na Aston Villa na baadae Chelsea kwenye uwanja wake wa nyumbani.

                                Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment