Usajili
wa wachezaji kwa dirisha dogo kwa msimu wa 2013/2014 Tanzania Bara unafunguliwa
Novemba 15 mwaka huu na utafungwa rasmi Desemba 15 mwaka huu.
Kwa
mujibu wa kanuni, klabu zenye fursa ya kusajili wachezaji katika dirisha dogo
ni zile ambazo hazijatumia nafasi zote 30 za wachezaji.
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zimemaliza duru la kwanza
msimu huu. Duru za pili litaanza kutimua vumbi Januari mwakani.
Kwa
mujibu wa Kalenda ya Matukio ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
matukio ya Novemba na Desemba ni dirisha dogo la usajili na mechi za kirafiki
za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date.
Matukio
mengine ni michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini
ya miaka 20 wa klabu za VPL na michuano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika
Nairobi, Kenya.
Boniface
Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu
Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment