Pages

Ads 468x60px

Friday, November 8, 2013

MBEYA CITY:-



Hii ni kati ya timu ambazo zimewafurahisha mashabiki wa soka si mkoani Mbeya pekee bali Tanzania nzima.
Soka la uhakika,kujiamini ni mmoja ya sababu kubwa iliyowafanya wajizolee mashabiki wengi kila wanapokanyaga katika ardhi ya  mkoa wowote hapa Tanzania wakiongozwa na kocha mzoefu Juma Mwambusi.
Sikushangaa kusikia mashabiki wao ni wakorofi ,wahuni au vinginevyo nadhani hii ilinikumbusha usemi usemao mti wenye matunda ndio hupigwa mawe.
Ni kweli mchezo wa soka umetawaliwa na nidhamu kuanzia nje hadi ndani ya uwanja lakini si kila mtu amekamilika chakuwaomba mashabiki wa Mbeya City  waishangilie timu yao popote na kwa style yeyote bila kuvuruga amani yasije yakawakuta yaliyowakuta Simba.
Swali ninalojiuliza ni je, Simba, Yanga, Azam, Coastal Union na Kagera Sukari watakubali kupelekwa puta duru ijayo au kuna mipango ya kuibomboa Mbeya City wasiendelee kuadhiriwa na kikosi hichi chenye kiu ya mafanikio?

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment