Pages

Ads 468x60px

Sunday, November 17, 2013

TEMBO WA IVORY COAST WAIFUATA NIGERIA KATIKA KOMBE LA DUNIA MWAKANI NA KUWA TAIFA LA PILI BARANI AFRIKA KUFUZU KWA MICHUANO HIYO.

Timu ya soka Ivory Coast  imekuwa timu ya pili kutoka barani Afrika kufuzu fainali zijazo za kombe la dunia baada ya usiku wa jana kutoka sare ya kufungana goli 1 kwa 1 na Segegal katika mchezo wa maruadiano kufuzu kwa fainali hizo zitakazo fanyika mwakani nchin Brazil.

Ivory Coast maarufu mama Tembo iliwabiadi wasubiri daika tatu za nyongeza baada ya kumalizika zile 90 ikiwa nyuma kwa goli mmoja  ndipo Solomon Kalou kuisawazishia timu yake likiwa ni shambulizi la mwishoni kwa Tembo hao kwenye mchwezo huo uliochezwa nchini Burkinafaso.

Senegal ilijipatia bao lake kwa mkwaju wa penalti iliyopigwa kwa ufundi mkubwa na Mussa Sow kunako dakika ya 77 bao ambalo liliamusha ari kubwa kwa Simba hao wa Teranga kutaka kupindua matokeo ya awali ambapo walifungwa magoli 3 kwa 1 kwenye mchezo kwanza nchini Ivory Coast.

Katika hatua nyingine kivumbi cha michuano hiyo ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia kwa mataifa ya Afrika leo kuna mchezo mwengine baina ya Cameroon na Tunisia ambapo Cameroon itakuwa mwenyeji wa mchezo huo.

katika mchezo wa awali timu hizo hazikufungana nchini Tunisia na keshokutwa Misri itakuwa mwenyeji wa Ghana.

                                         Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment