Na
Issa Maeda.
Huenda
hili ndio kengeza langu.
Mapacha watatu wanoshabihiana kwa
sifa bainifu timu ya taifa ya england , bafana bafana na ndugu yao taifa
stars', kwaheshima tutaanza na watawala wetu huenda wao ndio walioturithisha
ujinga huu kwa fikra zangu england wanaongoza kwa visingizio kila baada ya
mashindano fulani baada ya kutolewa kwenye kombe la mataifa ya ulaya 2004
walimlaum sana jorge andrade kwa kuwafanya
wafute ndoto yao ya kutwaa kombe la mataifa ya ulaya baada ya kumuumiza mguu
nyota wao shujaa wao mwenye umri mdogo wayne rooney kwenye mchezo wa robo
fainali ya kombe la mataifa ya ulaya lililoandaliwa nchini ureno hivyo england
alitolewa na wenyeji kisha wakapata sababu ya kuongelea kwenye media house,
2006 wakapata nafasi kushiriki kombe la dunia lillilofanyika nchini ujerumani
lakini walipokutana na ureno england walipata tena sababu nyingine ya kutoka
kwenye michuano baada cr7, kuonekana ndio sababu ya wao kutolewa kwenye
michuano kisa alimshtakia rooney kwa refa baada ya rooney kumchezea vibaya
ricardo calvaro na rooney akapewa kadi nyekundu na mwisho wa siku ureno
walipita england wakirejea nyumbani na kisingizio cha ronaldo walimchukia na
walitishia kumuua, 2008 hawakuwa na jipya fainali za euro walizisikia tu ila
2010 walirejea tena safari hii walikutana na kisanga kikubwa mbele ya timu ya
taifa ya ujerumani england walizidiwa kila idara mesut ozil tomas muller
waliwakimbiza simba watatu mwisho wa siku england alifungwa 4 kwa 1 na kutolewa
kwenye mashindano kisingozio kikabaki refa alikataa goli la lampard wakawashawishi
wananchi waamini kama goli la lampard lingekubaliwa wangevuka kizingiti cha
ujerumani hawakuishia hapo wakawashawishi fifa kuangalia uwezekano wa kuleta
goal line technology ilikuondoa utata wa magoli kama la lampard, nahisi
wakitolewa kwenye robo fainali ya kombe la dunia 2014 watakuja na sababu
nyingine itakayoleta mjadala pia wanaweza kutumia sababu ya kushindwa kumtumia
mchezaji flani kama ngao yao ya kujilinda na maadui usishangae wakakwambia
hatujasonga mbele kisa januzaj kakataa kuichezea england, leo wamenifurahisha
wanaunda kamati itakayoisaidia england itwae kombe la dunia 2022 nchini qatar
nawaunga mkono kwa asilimia 100 kwa mpango mkakati huu ila wasisahau kuwa wao
hawana vipaji ila wanaweza kutumia njia au sera moja wapo iliyotumiwa na
wakoloni wa kifaransa kuwatawala waafrika asimilation kupata vipaji kutoka
mataifa yaliobarikiwa ili kuijenga timu ya taifa ya simba watatu, afrika kusini
wanatumia sana vyombo vya habari kujitangaza lakini mara ya mwisho kuwaona
kwenye kiwango bora ni ule mwaka 1996 walipotwaa kombe la mataifa ya afrika
wakiwa na nyota kama lukas radebe, piere issa, dr khumalo adreas arenze wengine
kibao baada ya hapo wamekuwa waandaaji wa makombe ila imebaki ndoto kwenye
kuyachukua afrika kusini wanaligi bora kama ilivyo england ligi ya afrika
kusini ni ya tano kwa utajiri lakini wachezaji wengi wenye vipaji wanatoka nje
ya nchi yao hivyo bafanabafana wataendelea kuwa wanyonge kutokana na sera mbovu
za shirikisho la soka la nchi hiyo waangalie wapi wanajikwaa ili kuweza
kuondokana na uozo kwenye timu ya taifa, wiki iliyopita kocha wa timu ya taifa
ya tanzania kim paulsen aliviita vikosi viwili vya taifa stars kimoja cha
zamani na future taifa stars kilichonishangaza alimwita golkipa ivo mapunda
kwenye kikosi cha future taifa stars hahaha blaza anaumri unaozidi miaka 40 ni
vipi atakuwa future au tegemeo la baadae kwenye taifa ambalo mara ya mwisho
tulicheza fainali za kombe la mataifa ya afrika mwaka 1980, leo unakiita kibabu
kiwe future tunataka future ipi ambayo sio ya kina dilunga, sio ya kina paul
nonga, ambayo sio ya kina aishi manula, sio ya kina msuva? Kama ivo ni future
tumrejeshe nsajigwa kutoka kwenye kustaafu aje awe future yetu, najiuliza mbeya
city ya juma mwambusi na master mind maka mwaluisi hawana mchezaji anayeweza
kuisaidia stars kwenye hiyo future, waliwezaje kushika nafasi ya 3 kwenye ligi
waliwezaje kutoruhusu kutofungwa magoli mengi waliwezaje kuwa moja ya timu
zizoshindikana kufungwa mzunguko wa kwanza, inamaana mbeya city haina nyota
angalau wawili kuisaidia future? lakini ghafla usingizi inaniruka na kumbukumbu
zinanirejea kuwa pamoja na kuwa na mkurugenzi wa ufundi pale tff hana uzalendo
na taifa hili leseni yake ya fifa haitusaidii kuondokana na matatizo yetu,
tutabadilisha sana makocha hata tukimpa arsene wenger taifa stars itaendelea
kuwa bichwa la mwenda wazimu kwakuwa hatujajua kinachotula kipo nguoni mwetu,
mkurugenzi hamtembezi kocha mikoani kujua wachezaji wapya hakuna sera za
kuendeleza vipaji kuanzia kata tarafa hadi taifa, tutaishia kulaumiana tu, kama
walivyoamka leo england tukaechini tujue tatizo letu nn kisha tutatue mapema ss
na afrika kusini na england tuna matatizo yanayofanana, huenda tunaligi bora
ila wachezaji wazawa hawana ubora, pia hatuna njia mbadala ya kuzalisha vipaji
vipya, au vinavyozalishwa havina muendelezo mzuri,. Tukishindwa tuanzishe kombe
letu tuwe tunashiriki tanzania england na afrika kusini labda tunaweza kupata
mshindi.
Posted by Yusuph Mkule.
No comments:
Post a Comment