Pages

Ads 468x60px

Saturday, November 23, 2013

ARSENAL YAZIDI KUJIIMARISHA KILELENI MWA MSIMAMO WA LIGI,LIVERPOOL YAPUNGUZWA KASI.




Timu ya soka ya Arsenal imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya nchini England baada ya hii leo kuinyuka Southampton magoli 2 kwa 0 kwenye uwanja wake wa nyumbani Emirates nakuendelea kuongoza kwa alama 28 baada ya kucheza michezo 12 hadi hivi sasa.

magoli yote mawili ya Arsenal hii leo yameshindiliwa kimiani na mchezaji Olivier Giroud kunako dakika ya 22  baada ya kumpokonya mlinda mlango wa Southampton Artur Boruc ambae alishindwa kuumiliki mpira aliorudishiwa na beki wake hivyo kuizawadia Arsenal goli la kwanza.

Hadi mapumziko Arsenal ilikuwa mbele kwa goli hilo 1.Arsenal ambayo hii leo ilifurahia ujio wa Theo Walcotti ambaye alikuwa majeruhi ilipata goli la pili kunako dakika ya 86 kwa mkwaju wa Penalti uliokwamishwa nyavuni na Giroud na kisha kuufanya mchezo huo kumalizika kwa Arsenal kushinda magoli 2 kwa 0 dhidi ya wapinzani wao.
katika mchezo huo Arsenal ilitawala kwa asilimia 51 huku Southampton ikitawala kwa asilimia 49.

kwamatokeo hayo Arsenal inaendelea kuongoza ligi kwakufikisha alama 28 huku Liverpool baada ya kulazimisha sare ya kufungana magoli 3 kwa 3 na Everton ikishika nafasi ya pili kwakuwa na alama 24 huku Southampton baada ya kufungwa na Arsenal imepunguzwa kasi na sasa inashika nafasi ya tatu kwakuwa na alama 22.
matokeo mengine kwa michezo iliyomalizika  hii leo Fulham imefungwa magoli 2 kwa 1 na Swansea City,Crstal Palace ikiwa na kocha wake mpya Tony Pulis ikafanikiwa kupata ushindi wa pili tangu kuanza kwa msimu huu baada ya kuifunga Hull City goli 1 kwa 0.

Newcastle United ikiwa nyumbani imefanikiwa kushinda magoli 2 kwa 1 dhidi ya Norwich ilihali Stock City ikiutumia vyema uwanja wake wa nyumabni baada ya kuifunga Sunderland magoli 2 kwa 0. mchezo mwingine katika ligi kuu ya England unazikutanisha Chelsea ambayo imesafiri kuifuata Westham United,utam wa mchezo huo ni kutokana na timu zote kutoka katika jiji la London.

                                      Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment