Pages

Ads 468x60px

Wednesday, November 20, 2013

NAHODHA WA TIMU YA TAIFA YA SWEDEN AIVULIA KOFIA URENO BAADA YA KUWARARUA USIKU WA JANA.



Mshambuliaji wa PSG na nahodha wa timu ya taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimovic ameeleza masikitiko yake kwa taifa lake kushindwa kufuzu fainali zijazo za kombe la dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.
Akizungumza baada ya timu yake ya taifa kunyukwa magoli 3 kwa 2 na Ureno kwenye ardhi yao ya nyumbani Ibra amesema kwanza anaipongeza Ureno kwa kupata nafasi hiyo ambayo wote walikuwa wakiiwania.
Zlatan ambaye ameshiriki fainali za kombe la dunia mara mbili tuu katika historia yake ya soka fainali za 2002 na za 2006 ameiambia tovuti ya Uefa kuwa sababu kubwa ya wao kutolewa na Ureno ni kutokana na kikosi cha Ureno kuwa bora zaidi yao.
Sweden ambayo imetolewa kwa uwiano wa magoli 4 kwa 2 na Ureno nahodha wao amesema wanapaswa kutazama makosa waliyoyafanya lakini katika soka lolote laweza kutokea na kuongeza kuwa wamefungwa kutokana na makosa waliyoyatenda.
Katika mchezo wa jana ambao ulikuwa kama kipimo cha Zlatan na Ronaldo mreno huyo ameonyesha ubora wake baada ya kufunga magoli yte matatu kwenye pambano hilo huku Zlatan akiifungia Sweden magoli yao mawili.

Mbali na Ureno mataifa mengine ya Ulaya  yaliyofuzu fainali zijazo za kombe la dunia hapo jana ni Ufaransa ambayo iliifunga Ukrain magoli 3 kewa 0,Ugiriki iliyopita kwa uwiano wa magoli 4 kwa 2 dhidi ya Roamania kufuatia kutoka sare ya goli 1 kwa 1.
Croatia pia imefuzu fainali hizo baada ya kuiadhibu Iceland magoli 2 kwa 0.

BARANI AFRIKA.

Ghana yenyewe hapo jana imejipatia tiketi ya kwenda Brazil licha ya kunyukwa magoli 2 kwa 1 na mafarao wa Misri  mchezo ulichezwa na kupatiwa ulinzi mkali wa askari waliokuwa wametanda kila kona.
Mbweha wa jangwani Algeria wakajipatia tiketi ya kwenda Brazil baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1 kwa 0 mbele ya Burkinafaso na kukamilisha mataifa matano ya Afrika yatakayoshiriki fainali hizo.
Mataifa 32 yaliyofuzu kwa fainali hizo mwakani kutoka kila bara ni kama ifuatavyo.
Kutoka Afrika ni Nigeria,Ivory coast,Cameroon,Ghana na Algeria.
 

Asia: Australia, Iran, Japan, South Korea
Ulaya : Belgium, Bosnia-Hercegovina, Croatia, England, France, Germany, Greece, Italy, Netherlands, Portugal, Russia, Switzerland, Spain
Amerika ya kaskazini na Caribbean: Costa Rica, Honduras, United States
America kusini: Argentina, (wenyeji) Brazil, Colombia, Ecuador, Chile.
Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment