TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Novemba
21, 2013
Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim
Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya Kombe la
Chalenji inayofanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 27 mwaka huu.
Kilimanjaro Stars iliyotwaa kombe
hilo mara ya mwisho mwaka 2010 chini ya Kocha Jan Poulsen, na ambayo imepangwa
kundi B katika michuano ya mwaka huu itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28
mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos.
Wachezaji wanaounda kikosi hicho cha
Tanzania Bara ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia,
Kenya) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam),
Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na
Said Moradi (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba),
Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan
Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Safu ya ushambuliaji inaundwa na
Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma
Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na
Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Kilimanjaro Stars inatarajia
kuondoka Jumatatu (Novemba 25 mwaka huu) kwenda Nairobi kushiriki michuano hiyo
itakayoanza Novemba 27 mwaka huu na kumalizika Desemba 13 mwaka huu.
MECHI DHIDI YA STARS, ZIMBABWE
YAINGIZA MIL 50/-
Mechi ya kirafiki ya kimataifa ya
FIFA Date kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe (The Warriors) iliyochezwa
juzi (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh.
50,980,000 kutokana na watazamaji 7,952.
Tiketi za kushuhudia mechi hiyo
ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama
ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 7,776,610.17
wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 3,682,560.
Asilimia 15 ya uwanja sh. 5,928,124,
asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 7,904,166 na asilimia 5 ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 1,976,041.
Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 17,784,373 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar
es Salaam (DRFA) sh. 889,219 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF)
Posted by Yusuph Mkule.
No comments:
Post a Comment